Jumapili Tarehe 6/04/2014 litafanyika Tamasha kwa ajili ya kuwategemeza watoto yatima wa kituo cha HOTECH Kimara. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Kanila La Baptist Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam, Tanzania. 

Kutakuwa na waimbaji wa nyimbo za Injili mbalimbali wakiongozwa na Rose Muhando. Waimbaji wengine watakao hudumu katika Tamasha hilo ni Janeth Mrema, Sifa John, Addo Novemba, Faraja Ntaboba, Christina Matai, Stela Joel na wengineo.

Hakutakuwa na kiingilio ila watu wote mtakao hudhuria Tamasha hilo mnashauriwa kuja na zawadi mbalimbali kama vile nguo, viatu, daftari, karamu, chakula na nyinginezo kwa ajili ya kusaidia watoto yatima kwa kadri mtakavyoguswa.


0 comments:

Post a Comment

 
Top