Kituo cha Radio cha Kwa Neema FM Radio kinachoangaza jijini Mwanza jumapili hii tarehe 30/03/2014 katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuanzia saa 5 asubuhi kimefanya sherehe za maadhimisho ya miaka minne tangu kuanza kurusha matangazo yake kanda ya ziwa. Katika sherehe hizo Kwa Neema FM Radio iliwashirikisha wadau mbalimbali toka kanda ya ziwa na vitongoji vyake na kwingineko ndani na nje ya Tanzania.


Waimbaji mbalimbali kama vile; Edson Mwasabwite, Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Stara Thomas, AIC Nyakato, Kwa Neema Band na wengineo walishiriki.

Edson Mwasabwite Akiimba Ni Kwa Neema Na Rehema



Bahati Bukuku akitumbuiza


Flora Mbasha akimsifu Mungu

Stara Thomas akimwimbia Mungu


Mitambo na vifaa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo vilikuwa ni vyenye ubora na kiwango kizuri.


Wadau na wajasiliamali mbalimbali pia walipata fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zao katika sherehe hizo.


Watangazaji wa Kwa Neema FM Radio


Watangazaji wa Kwa Neema FM Radio



0 comments:

Post a Comment

 
Top