Habari za kuhuzunisha ambazo zimetokea jana Jumapili mchana ni juu ya kufariki kwa mwimbaji wa Muziki wa Injili Peter Kaberere.

Zikitolewa na Groove Awards taarifa zilisema:

"It is with heavy hearts that we confirm that our brother 'Kabz' Anthony Peter Kaberere has gone home to be with the Lord. Gone too soon. Pray for his family"
Its with heavy hearts that we confirm that our brother ‘Kabz’ Antony Peter Kaberere has gone home to be with the Lord. Gone too soon..pray for his family. - See more at: http://www.ulizalinks.co.ke/sad-gospel-artist-kaberere-passed/#sthash.DJg7XhW9.dpuf


Kaberere alikuwa msanii injili & mkuu wa vifaa katika Mo Sound Limited ambao ni waandaaji wa tuzo za Injili Za Mwaka Groove Awards. Kaberere alianza muziki wa Injili katika Zaidi Ya Muziki ( Jogg C ) na baadaye akaanza kuimba kwa kujitegemea. Akiwa muimbaji wa kujitegemea alifanikiwa kutoa nyimbo kama vile 'Kiburi', 'Natamani' alishirikiana na Eunice Njeri, 'Just A Way' akishirikiana na Mr Vee na 'Mwanamke' alioutoa hivi karibuni. 

Kaberere alikuwa mbioni kutoa video yake mpya ya wimbo uitwao 'Mitego' mwezi huu wa Aprili iliyoongozwa na J Blessing. Kifo cha Kaberere kilisababishwa na shoti ya umeme katika gari lake alipokuwa analiosha siku ya Jumapili mchana. 

Ameacha mke ambaye anajulikana na wengi katika hii tasnia ya muziki wa Injili kama "Njesh Wa Kabbz" na mtoto wa kiume.

1 comments:

Unknown said... April 7, 2014 at 10:29 AM

I am sad you are gone! Rest In Peace Kaberere!

Post a Comment

 
Top