Muimbaji wa Muziki wa Injili ndugu Upendo Kilahiro athibitishwa kushiriki katika Mkesha Maalumu Wa Muziki Wa Pasaka utakaofanyika Baracuda Beach Kigamboni, Dar es Salaam siku ya Ijumaa ijayo tarehe 18 kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi. 


Mkesha Wa Muziki Wa Pasaka ni maalumu kwa Nyimbo na jumbe nzito sana za kuhusu kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu.

Katika post zake kwenye event page maalumu ya mkesha huo mmoja wa waandaaji wa Mkesha Maalumu Wa Muziki Wa Pasaka ndugu Abel Orgenes Ijengo  amesema “Tutakuwa na dada Upendo Kilahiro....na wengine nitaendelea kuwataja kadri wanavyo confirm”


Pamoja na muandaaji mwenyewe ndugu Abel Orgenes Ijengo, wengine watakaoshiriki katika mkesha huo ni waimbaji mahiri na wapiga vyombo live ‘The Patmos’ kutoka Kigamboni ambao wamekuwa wakishiriki tangu kuanza kwa matukio haya ya Injili ya maalumu ya kuifikia Kigamboni kwa Upendo wa Yesu chini ya kiongozi mwenye moyo mzuri wa Kitumishi na Vipaji lukuki ndugu Godwin.

Watu wote kutoka Kigamboni na kwingineko jijini Dar es Salaam na ndani na nje ya nchi ya Tanzania mnakaribishwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top