Mtumishi wa Mungu muimbaji wa Muziki wa Injili, Rose Mutiso anatarajia kuzindua DCD/VCD ya albam yake ya tatu hivi karibuni. Uzinduzi huo utafanyika AIC ATHI RIVER, Nairobi, Kenya Tarehe 27, Aprili, 2014 kuanzia saa 8 mchana.



Wanamuziki wa Nyimbo za Injili watakao msindikiza ni Jeremiah Mulu, Victor Mbagga, Jasto Mwangangi, David Mpanilehi and Winnie Mutanu. Wengine ni Mirriam Mutindi, Bretta Kimathi, Maggie Mutunga, Catherine Kioko, Dorcas Kyalo, Elizabeth Nyanzi, Veroh, Grace Makau, Joy Nargaret, Getruda Ngassa, AIC Athiriver Kiswahili Choir, Upendo Women Choir, Vijana Choir, English Choir, English Choir na wengineo

Albam inayozinduliwa inaitwa LINDA MOYO ambayo ina nyimbo kumi (10) ambazo ni Linda Moyo, Ifike Wakati, Arusi, Tumaini, Nitatangaza, Mpeni Bwana, Shika Shikilia, Ni Bwana, Wapenda Kubembelezwa, na Je Tutapataje Kupona.

Albamu ya kwanza ya Mtumishi Rose Mutiso inaitwa WACHUNGAJI SIKIENI na ya pili inaitwa AMENITUMA ambazo zote ziko katika mifumo ya Audio na Video na zinapatikana sokoni nchini Kenya, Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Video za albamu ya LINDA MOYO zimefanywa na kampuni ya MBC HOT MEDIA yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Rose Mutiso amehudumu sehemu mbalimbali nchini Kenya na katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga nchini Tanzania na yuko tayari kuhudumu na kutumika kama Baraka katika mikutano na matamasha mbalimbali yanayomtukuza Mungu popote pale.

0 comments:

Post a Comment

 
Top