Mwanzilishi na mchungaji wa SHERKINAH GLORY WORSHIP TABERNACLE nchini Afrika Kusini, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Black Pearl Media, Mshindi wa tuzo mbalimbali za muziki wa Injili ambaye ametoa CD na DVD zilizofikia mauzo ya platnum na kusambaa kote Afrika, Muigizaji wa ukumbini na Mchezaji anayejulikana kama Keke, Kekeletso Phoofolo, Jumapili iliyopita aliungana na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka Tanzania, Kenya, Zambia na Uingereza katika kumsifu Mungu siku ya Pasaka katika Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam likiandaliwa na Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake ndugu Alex Msama.
Miongoni mwa wanamuziki waliotumbuiza katika
tamasha hilo ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka
Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Rose Muhando.
Katika
Tamasha hilo mgeni rasmi alikua ni Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania mh.Bernad
Membe ambaye alimuwakilisha rais Jakaya Kikwete kutokana na kutoweza kuhudhuria
kwa kuwa nje ya nchi kwa shughuli za kiserikali.
Utukufu ni kwa Bwana aliyeubariki ulimwengu na kumpa kipawa mtu huyu na nafasi ya kuonyesha kipawa chake hicho kisicho na kifani katika nchi ya walio hai. Sio tu kipaji kilicho katika mzunguko wa damu na katika mishipa yake, lakini pia nguvu ya Mungu kupitia muziki wake ambayo inamtofautisha yeye na wasanii wengine.
Keke akisalimiana na Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania |
Utukufu ni kwa Bwana aliyeubariki ulimwengu na kumpa kipawa mtu huyu na nafasi ya kuonyesha kipawa chake hicho kisicho na kifani katika nchi ya walio hai. Sio tu kipaji kilicho katika mzunguko wa damu na katika mishipa yake, lakini pia nguvu ya Mungu kupitia muziki wake ambayo inamtofautisha yeye na wasanii wengine.
Tumbuizo lilikuwa zuri ni wimbo baada ya wimbo baada ya wimbo |
Wakati Afrika Kusini ... ilikuwa imechoka na Tunes zilizozoeleka katika muziki wa injili, Keke aliwasili na kuleta dhana tofauti kwa kuuleta muziki wa Injili kwa vijana kwa jinsi inayowafaa. Kubadilika kwake juu ya jukwaa humfanya kila mmoja kustaajabu na kuvutiwa na muziki wa Injili.
Keke, ambaye jina lake halisi
ni Kekeletso Phoofolo , alizaliwa na kukulia Pimvill , Soweto. Akiwa
na umri wa zaidi ya miaka 30 mwimbaji ambaye akiwahi kuwa na bidii ya kuwa
katika jeshi lakini muziki alichukua nafasi na kumfanya kuanza kazi yake na Zoe
Gospel Music mwaka 1994 kama “backing vocalist” na baadae kukamilisha kwenye
"Shell Road to Fame " Sun City mwala
1997 kama mkongwe.
Back Vocalists wakimsindikiza Keke katika Tamasha la Pasaka |
Katika kuhudumu kwake na kutafuta kibali Keke amefanya kazi na wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bheki Mseleku, Winston Mankunku na Umoja . Hii ilisababisha simu kutoka kwa Malkia wa Swaziland kuongoza na kusimamia "live" recording ya Redemption Choir mwaka 2001-2004 na kumpatia nafasi zaidi za kufanya “projects” katika nchi za jirani.
Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anahudu kwa kipawa chake |
Mwaka 2006 aliamua kuimba kama solo ambayo ilifanya vizuri. Mafanikio ya albamu yake ya kwanza iitwayo ‘Restoration’ (Matengenezo) iliandaa njia kwa ajili ya albamu yake ya pili 'Revival (Uamsho)' ambayo ilikuwa 'Live' DVD iliyorekodiwa "Vaal University of Technology” (Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Vaal).
Kwenye UAMSHO,
Keke ambaye ni mume wa mke mmoja na baba wa watoto
watatu anasema 'Sote tuna nafasi ya kuwa na tunachotaka,
na tunachohitaji kufufua
akili zetu. Hisia lazima zishughulikiwe kwa sababu tuna uhuru wetu na Afrika
ina zaidi ya inavyohitaji. Tuje nje ya mawazo ya kimaskini. Huu
si wakati wa kuangalia nyuma kwa
sababu kama tukifanya hivyo,
hatutaweza kuiona kesho.” DVD hiyo ina ya nyimbo nzuri
kama vile Sefapano, ‘I’m in Love’, ‘I need Your Touch’
na ‘Testimony’ to mention few of the best in his live album.
Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria Tamasha la Pasaka |
Album
zilizorekodiwa “live” ambazo Keke amefanya katika huduma yake ya Muziki wa
Injili ni Revival, Living Testimony, Holy of Hollies na Spirit Unlimited.
0 comments:
Post a Comment