Mwisho wa wiki hii utakuwa ni wa Baraka na furaha kwa wakaazi na watu wote waliopo jijini Dar es Salaam  Tanzania kwa kuwa Bwana amewapa nafasi ya kumshuhudia “live” mwanamuziki nguli wa Muziki wa Injili Joseph Ebhodaghe anayetambulika kama Joe Praise kutoka nchini Nigeria. Kwa wakazi wa Dar es Salaam hii ni nafasi nyingine tena kwao kutembelewa na waimbaji maarufu wa muziki wa Injili baada ya wiki iliyopita kutembelewa na Keke kutoka Africa Kusini.


Joe Praise ambaye anatamba sana na wimbo wake uitwao Mighty God ambao alishirikiana na Soweto Gospel Choir ya Afrika Kusini amekubalika na kupata mafanikio mbalimbali katika huduma yake ya uimbaji ikiwemo mialiko kutoka ndani na nje ya nchi yake ya Nigeria.

Tayari Joe Praise amewasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini Marekani ambako hufanyia shughuli zake muda mwigi tayari kuhudumu katika Faith Miracle Seminar’ itakayoendeshwa na HEALING MINISTRATION chini ya mtumishi Pastor Ken Igini. Semina hiyo kubwa pamoja itafanyika kwa muda wa siku tatu (Ijumaa Tarehe 25/04/2014 hadi Jumapili Tarehe 27/04/2014) katika ukumbi wa CHRIST EMBASSY TANZANI (Twiga Sunset Hall), Makonde, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 10:30 jioni.



0 comments:

Post a Comment

 
Top