Friday, April 25, 2014

JOE PRAISE KUHUDUMU JIJINI DAR ES SALAAM


Mwisho wa wiki hii utakuwa ni wa Baraka na furaha kwa wakaazi na watu wote waliopo jijini Dar es Salaam  Tanzania kwa kuwa Bwana amewapa nafasi ya kumshuhudia “live” mwanamuziki nguli wa Muziki wa Injili Joseph Ebhodaghe anayetambulika kama Joe Praise kutoka nchini Nigeria. Kwa wakazi wa Dar es Salaam hii ni nafasi nyingine tena kwao kutembelewa na waimbaji maarufu wa muziki wa Injili baada ya wiki iliyopita kutembelewa na Keke kutoka Africa Kusini.


Joe Praise ambaye anatamba sana na wimbo wake uitwao Mighty God ambao alishirikiana na Soweto Gospel Choir ya Afrika Kusini amekubalika na kupata mafanikio mbalimbali katika huduma yake ya uimbaji ikiwemo mialiko kutoka ndani na nje ya nchi yake ya Nigeria.

Tayari Joe Praise amewasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini Marekani ambako hufanyia shughuli zake muda mwigi tayari kuhudumu katika Faith Miracle Seminar’ itakayoendeshwa na HEALING MINISTRATION chini ya mtumishi Pastor Ken Igini. Semina hiyo kubwa pamoja itafanyika kwa muda wa siku tatu (Ijumaa Tarehe 25/04/2014 hadi Jumapili Tarehe 27/04/2014) katika ukumbi wa CHRIST EMBASSY TANZANI (Twiga Sunset Hall), Makonde, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 10:30 jioni.



Thursday, April 24, 2014

MFAHAMU KEKE: MUIMBAJI KUTOKA AFRIKA KUSINI ALIYETIA FORA KATIKA TAMASHA LA PASAKA


Mwanzilishi na mchungaji wa SHERKINAH GLORY WORSHIP TABERNACLE nchini Afrika Kusini, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Black Pearl Media, Mshindi wa tuzo mbalimbali za muziki wa Injili ambaye ametoa CD na DVD zilizofikia mauzo ya platnum na kusambaa kote Afrika, Muigizaji wa ukumbini na Mchezaji anayejulikana kama Keke, Kekeletso Phoofolo, Jumapili iliyopita aliungana na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka Tanzania, Kenya, Zambia na Uingereza katika kumsifu Mungu siku ya Pasaka katika Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam likiandaliwa na Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake ndugu Alex Msama.

Kekeletso Phoofolo (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Tamasha la Pasaka.

Miongoni mwa wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Rose Muhando.

Katika Tamasha hilo mgeni rasmi alikua ni Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania mh.Bernad Membe ambaye alimuwakilisha rais Jakaya Kikwete kutokana na kutoweza kuhudhuria kwa kuwa nje ya nchi kwa shughuli za kiserikali.

Keke akisalimiana na Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Utukufu ni kwa Bwana aliyeubariki ulimwengu na kumpa kipawa mtu huyu na nafasi ya kuonyesha kipawa chake hicho kisicho na kifani katika nchi ya walio hai. Sio tu kipaji kilicho katika mzunguko wa damu na katika mishipa yake, lakini pia nguvu ya Mungu kupitia muziki wake ambayo inamtofautisha yeye na wasanii wengine.

Tumbuizo lilikuwa zuri ni wimbo baada ya wimbo baada ya wimbo

Wakati Afrika Kusini ... ilikuwa imechoka na Tunes zilizozoeleka katika muziki wa injili, Keke aliwasili na kuleta dhana tofauti kwa kuuleta muziki wa Injili kwa vijana kwa jinsi inayowafaa. Kubadilika kwake juu ya jukwaa humfanya kila mmoja kustaajabu na kuvutiwa na muziki wa Injili.

Keke, ambaye jina lake halisi ni Kekeletso Phoofolo , alizaliwa na kukulia Pimvill , Soweto. Akiwa na umri wa zaidi ya miaka 30 mwimbaji ambaye akiwahi kuwa na bidii ya kuwa katika jeshi lakini muziki alichukua nafasi na kumfanya kuanza kazi yake na Zoe Gospel Music mwaka 1994 kama “backing vocalist” na baadae kukamilisha kwenye "Shell Road to Fame " Sun City mwala 1997 kama mkongwe.



Back Vocalists wakimsindikiza Keke katika Tamasha la Pasaka
Keke kamwe hakuwa akijizuia mwenyewe; mwaka 1998 aliingia katika Kwaito na kundi la watu walioitwa Kom - Kom . Kisha alipata fursa ya kwenda kwenye ziara na Benjamin Dube 1999 kabla ya kujiunga na " Joyous Celebration 5" mwaka 2000-2001 kama mojawapo wa waimbaji viongozi wa kwaya. Kuongoza kwake katika wimbo 'Jo Ke Mohlolo - Hlolo' kulimpa nafasi ya kufanya kazi na kundi wanaume la Redeemed. 

Katika kuhudumu kwake na kutafuta kibali  Keke amefanya kazi na wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bheki Mseleku, Winston Mankunku na Umoja . Hii ilisababisha simu kutoka kwa Malkia wa Swaziland kuongoza na kusimamia "live" recording ya Redemption Choir mwaka 2001-2004 na kumpatia nafasi zaidi za kufanya “projects” katika nchi za jirani.

Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anahudu kwa kipawa chake

Mwaka 2006 aliamua kuimba kama solo ambayo ilifanya vizuri. Mafanikio ya albamu yake ya kwanza iitwayoRestoration’ (Matengenezo) iliandaa njia kwa ajili ya albamu yake ya pili 'Revival (Uamsho)' ambayo ilikuwa 'Live' DVD iliyorekodiwa "Vaal University of Technology” (Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Vaal).

Kwenye UAMSHO, Keke ambaye ni mume wa mke mmoja na baba wa watoto watatu anasema 'Sote tuna nafasi ya kuwa na tunachotaka, na tunachohitaji kufufua akili zetu. Hisia lazima zishughulikiwe kwa sababu tuna uhuru wetu na Afrika ina zaidi ya inavyohitaji. Tuje nje ya mawazo ya kimaskini. Huu si wakati wa kuangalia nyuma kwa sababu kama tukifanya hivyo, hatutaweza kuiona kesho.” DVD hiyo ina ya nyimbo nzuri kama vile Sefapano, ‘I’m in Love’, ‘I need Your Touch’ na ‘Testimony’ to mention few of the best in his live album.

Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria Tamasha la Pasaka

Album zilizorekodiwa “live” ambazo Keke amefanya katika huduma yake ya Muziki wa Injili ni Revival, Living Testimony, Holy of Hollies na Spirit Unlimited.

Wednesday, April 16, 2014

MTUMISHI WA MUNGU ROSE MUTISO KUZINDUA DVD/VCD ZA ALBAM YAKE YA TATU TAREHE 27, APRILI, 2014

Mtumishi wa Mungu muimbaji wa Muziki wa Injili, Rose Mutiso anatarajia kuzindua DCD/VCD ya albam yake ya tatu hivi karibuni. Uzinduzi huo utafanyika AIC ATHI RIVER, Nairobi, Kenya Tarehe 27, Aprili, 2014 kuanzia saa 8 mchana.



Wanamuziki wa Nyimbo za Injili watakao msindikiza ni Jeremiah Mulu, Victor Mbagga, Jasto Mwangangi, David Mpanilehi and Winnie Mutanu. Wengine ni Mirriam Mutindi, Bretta Kimathi, Maggie Mutunga, Catherine Kioko, Dorcas Kyalo, Elizabeth Nyanzi, Veroh, Grace Makau, Joy Nargaret, Getruda Ngassa, AIC Athiriver Kiswahili Choir, Upendo Women Choir, Vijana Choir, English Choir, English Choir na wengineo

Albam inayozinduliwa inaitwa LINDA MOYO ambayo ina nyimbo kumi (10) ambazo ni Linda Moyo, Ifike Wakati, Arusi, Tumaini, Nitatangaza, Mpeni Bwana, Shika Shikilia, Ni Bwana, Wapenda Kubembelezwa, na Je Tutapataje Kupona.

Albamu ya kwanza ya Mtumishi Rose Mutiso inaitwa WACHUNGAJI SIKIENI na ya pili inaitwa AMENITUMA ambazo zote ziko katika mifumo ya Audio na Video na zinapatikana sokoni nchini Kenya, Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Video za albamu ya LINDA MOYO zimefanywa na kampuni ya MBC HOT MEDIA yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Rose Mutiso amehudumu sehemu mbalimbali nchini Kenya na katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga nchini Tanzania na yuko tayari kuhudumu na kutumika kama Baraka katika mikutano na matamasha mbalimbali yanayomtukuza Mungu popote pale.